Trace Id is missing

Kipeto Lugha cha Kiolesura cha Windows 7

Kipeto Lugha cha Kiolesura cha Windows 7 (LIP) hutoa toleo lililofasiriwa nusu la Kiolesura cha Mtumiaji cha maeneo yanayotumika sana ya Windows 7

Muhimu! Kuchagua lugha hapa chini kutabadilisha maudhui kamili ya ukurasa kuwa lugha hiyo.

  • Toleo:

    1.0

    Tarehe Iliyochapishwa:

    14/1/2011

    Jina la Faili:

    LIP_sw-KE-32bit.mlc

    LIP_sw-KE-64bit.mlc

    Ukubwa wa Faili:

    2.5 MB

    4.0 MB

    Kipeto Lugha hiki Kiolesura cha Windows (LIP) hutoa toleo lililofasiriwa nusu la maeneo yanayotumika sana ya Windows. Baada ya kusanidi LIP, matini katika vigagula, vikasha ongezi, menyu, na mada za Msaada na auni zitaangazishwa katika lugha ya LIP. Matini ambayo hayajatafsiriwa yatakuwa katika lugha msingi ya Windows 7. Kwa mfano, kama ulinunua toleo la Kihispania la Windows 7, na ukasanidi LIP ya Kikatalani, matini mengine yatabaki katika Kihispania. Unaweza kusanidi zaidi ya LIP moja kwa lugha moja msingi. LIPs za Windows zinaweza kusanidiwa kwa matoleo yote ya Windows 7.
  • Mifumo ya Uendeshaji Inayotumika

    Windows 7

    • Microsoft Windows 7
    • Usanidi wa lugha msingi unaohitajika wa Windows 7: Kiingereza
    • 4.63 Mb ya nafasi huru ya kupakua
    • 15 Mb ya nafasi huru ya kusanidi

  • ONYO: Kama una usimbaji fiche wa BitLocker uliowezeshwa, tafadhali usitishe kabla ya kusanidi LIP. Fungua Control Panel, teua System and Security, kisha BitLocker Drive Encryption. Bofya kwenye Suspend Protection.

    Kwa sababu kuna vipakuaji vya kando vya matoleo ya 32-biti na 64-biti vya Windows 7 LIP, kabla ya kuanza kupakua, unahitaji kubainisha ni toleo lipi la Windows 7 ulilosanidi. Hivi ndivyo unavyostahili kubainisha ni toleo lipi la Windows 7 ulilosanidi:

    Bofya kwenye kitufe Start kisha bofya kulia kwenye Ngamizi na uteue Properties. Hii italeta maelezo msingi kuhusu ngamizi yako.
    Angalia katika sehemu ya Mfumo ya aina ya Mfumo. Hii itaashiria kama Mfumo wako Endeshi wa Windows 7 ni Mfumo Endeshi wa 32-biti au kama ni Mfumo Endeshi wa 64-biti.

    Kusanidi toleo la biti-32, aidha unaweza:

    1. Bofya kitufe cha Download, kisha bonyeza Open ili kusanidi LIP


    2. au

    3. Bofya Download pakua
      • Bofya Save ili kunakili jalada kwenye ngamizi yako,
      • Abiri kwa jalada lililopakuliwa na ulibofye mara mbili ili kusanidi LIP

    Kusanidi toleo la biti-64, lazima utumie chaguo la 2 hapo juu.