Trace Id is missing

Ufafanuzi wa Makubaliano yako ya Huduma

Tunasasisha Makubaliano ya Huduma za Microsoft, ambayo yanatumika kwenye bidhaa na huduma za mtandaoni za wateja wa Microsoft. Tunatengeneza visasisho hivi ili kufafanua masharti yetu na kuhakikisha kwamba yanabakia wazi kwako, na hata pia kusimamia bidhaa, huduma, na vipengele vipya vya Microsoft.

Visasisho hivi, ambavyo vimefupishwa hapa, vitaanza kutumika mnamo tarehe 30 Septemba, 2023. Ukiendelea kutumia bidhaa au huduma zetu baada ya tarehe 30 Septemba, 2023, utakuwa unakubaliana na masharti yaliyosasishwa ya Makubaliano ya Huduma za Microsoft.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je, Makubaliano ya Huduma za Microsoft ni nini?

Makubaliano ya Huduma za Microsoft ni makubaliano kati yako na Microsoft (au moja ya makampuni yake tanzu) ambayo yanasimamia matumizi yako ya bidhaa na huduma za wateja wa mtandaoni wa Microsoft. Unaweza kuona orodha kamili ya huduma na bidhaa zinazoshughulikiwa hapa.

Je, ni bidhaa na huduma gani zisizosimamiwa na Makubaliano ya Huduma za Microsoft?

Makubaliano ya Huduma za Microsoft hayatumiki kwenye bidhaa na huduma zinazowahusu wateja wanaotoa leseni kwa wingi, ikiwa ni pamoja na Microsoft 365 ya biashara, elimu, au wateja wa serikali, Azure, Yammer, au Skype ya Biashara. Kwa ahadi zinazohusiana na usalama, faragha na mwafaka na hata pia zinazohusiana na maelezo ambayo yanatumika kwa Kituo cha Imani cha Microsoft 365 cha biashara, tafadhali tembelea Kituo cha Imani cha Microsoft 365 kwenye https://www.microsoft.com/trust-center/product-overview.

Je, ni mabadiliko gani ambayo Microsoft inafanya katika makubaliano ya Huduma za Microsoft?

Tumetoa baadhi ya muhtasari wa mabadiliko yanayoonekana sana hapa.

Ili kuona mabadiliko yote, tunapendekeza usome Makubaliano yote ya Huduma za Microsoft.

Je, masharti haya yanaanza kutumika lini?

Visasisho hivi vya Makubaliano ya Huduma za Microsoft vitaanza kutumika mnamo tarehe 30 Septemba, 2023. Hadi wakati huo, masharti yako ya sasa yataendelea kutumika.

Ninawezaje kukubali masharti haya?

Kwa kutumia au kufikia bidhaa au huduma zetu baada ya tarehe 30 Septemba, 2023, utakuwa unakubaliana na Makubaliano yaliyosasishwa ya Huduma za Microsoft. Ikiwa hukubaliani nayo, unaweza kuchagua kutoendelea kutumia bidhaa na huduma na ufunge akaunti yako ya Microsoft kabla ya tarehe 30 Septemba, 2023.