Trace Id is missing

Muhtasari wa Mabadiliko ya Makubaliano ya Huduma za Microsoft – Septemba 30, 2023

Tunasasisha Makubaliano ya Huduma za Microsoft, ambayo yanatumika kwenye bidhaa na huduma za mtandaoni za wateja wa Microsoft. Ukurasa huu unatoa baadhi ya muhtasari wa mabadiliko yanayoonekana zaidi katika Makubaliano ya Huduma za Microsoft.

Ili uone mabadiliko yote, tafadhali soma Makubaliano kamili ya Huduma za Microsoft hapa.

  1. Katika kijajuu, tumesasisha tarehe ya chapisho kuwa tarehe 30 Julai, 2023, na tarehe ya kuanza kutumika kuwa tarehe 30 Septemba, 2023.
  2. Katika sehemu ya Faragha Yako, tulipanua ufafanuzi wa "Maudhui Yako" ili kujumuisha maudhui ambayo yanazalishwa na matumizi yako ya huduma zetu za AI.
  3. Katika sehemu ya Kanuni ya Maadili Mema, tuliongeza lugha ya kusimamia matumizi ya huduma za AI.
  4. Katika sehemu ya Kutumia Huduma na Msaada, tuliongezea yafuatayo:
    • Tuliongezea sehemu ya Usimamizi na Utekelezaji ili kufafanua na kuwasaidia watumiaji kuelewa vyema kanuni hizi.
    • Tuliongezea sehemu ya kuangazia haki zinazotolewa kwa wateja wa Australia wanaotumia bidhaa au huduma ambazo zinasimamiwa na Sheria ya Kuwalinda Wateja wa Huduma za Mawasiliano ambazo zinawaruhusu wateja kumchagua Mtetezi au Mwakilishi Aliyeidhinishwa wa kushughulika na Microsoft kwa niaba yao.
  5. Katika Shirika linalotoa Mkataba, sehemu ya Chaguo la Sheria, na Mahali pa Kutatua Mizozo, shirika linalotoa mkataba la sehemu za bila malipo za Microsoft Teams zimesasishwa kwa nchi ya Australia.
  6. Katika sehemu ya Masharti Maalum ya Huduma, tuliongezea na kufanya mabadiliko yafuatayo:
    • Tuliongezea rejeleo la Dynamics 365 kwa kuwa usajili wa majaribio wa bidhaa hii unaweza kuwezeshwa kupitia uhalalishaji wa akaunti ya Microsoft.
    • Tulibadilisha sehemu ya Bing Places ili kufafanua matoleo ya leseni ya mtumiaji ambayo itawezesha bidhaa kukidhi mahitaji ya utendakazi.
    • Tuliunda sehemu mpya inayoitwa "Hifadhi ya Microsoft" ambayo ina OneDrive na Outlook.com na huangazia mabadiliko ya chapa. Hii huangazia hali ya sasa ya viwango vya hifadhi ambapo viambatisho vya Outlook.com vinahesabika dhidi ya viwango vya hifadhi vya OneDrive na hata pia viwango vya hifadhi vya Outlook.com. Kiungo cha ukurasa chenye taarifa zaidi kimepeanwa pia.
    • Tulifafanua sehemu ya Microsoft Rewards kwa kuongezea maneno ya ziada yanayounga mkono matoleo ya mpango wa kimataifa, tukaongezea msaada wa kujisajili kiotomatiki kwa watumiaji wa akaunti ya Microsoft na mabadiliko mengine ya mpango, na maneno ya kuongezea ufafanuzi zaidi kuhusu mpango huu.
    • Tuliongezea sehemu ya huduma za AI ili kuweka vikwazo vingine, matumizi ya Maudhui Yako na mahitaji yanayohusishwa na matumizi ya huduma za AI.
  7. Katika sehemu ya Ilani, tumehariri ili kusasisha hali ya ilani ya leseni na hataza fulani.
  8. Katika Masharti yote, tumefanya mabadiliko ili kuboresha ufafanuzi na kushughulikia sarufi, uandishi, na matatizo mengine kama hayo. Tumesasisha pia kupeana majina na viungo vya wavuti.